
Kupatwa kwa mwezi
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo, imeeleza kuwa tukio hilo ni la kupatwa kwa mwezi sehemu (Penumbra), ambalo litaonekana katika nusu ya Dunia, hususani maeneo ambayo tarehe hiyo itakuwa usiku, ikiwemo Ulaya, Asia, Australia na Afrika.
Kwa mujibu wa TMA, hapa nchini hali hiyo imeonekana kuanzia jana, Julai 16 majira ya saa 3 hadi saa 9 usiku wa kuamkia Julai 17.
Aidha imeelezwa kuwa tukio hilo halina athari yoyote, ila upo uwezekano wa kuongezeka kwa kina cha maji katika bahari na kwamba hali hiyo inaelezwa kusababishwa na mvutano kati ya mwezi na maji katika bahari.