Friday , 30th May , 2014

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania mzee Kingunge Ngombare Mwiru amesema vyama vya siasa vya siasa nchini kikiwemo cha CCM ambacho yeye anatokea vinafanya siasa pasipo kujua vinapigania nini na kwa maslahi ya nani.

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, mzee Kingunge Ngombare Mwiru.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kitabu kinachoelezea namna ya ujengaji wa vyama vya siasa katika ngazi ya msingi nchini, mzee Kingunge amesema inasikitisha kuona kuwa vyama vya upinzani vimekuwa vikiendesha siasa za kutaka kuingia ikulu huku chama tawala kikifanya siasa za kutaka kubaki madarakani.

Kwa mujibu wa mzee Kingunge, vyama vya siasa vinatakiwa kuwa dira ya kutafuta suluhisho la mahitaji mbalimbali ya wananchi ikiwa ni pamoja na kutambua wapi nchi inataka kwenda kama ambavyo wao walifanya wakati wa harakati za kudai uhuru kutoka kwa wakoloni.