Makao makuu ya jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro.
Akiongea na wanahabari leo Oktoba 17, mkoani humo Kamanda Koka amesema tukio hilo limetokea Oktoba 15 katika Kata ya Kingachi wilayani Rombo, ambapo Daniel alivunja mlango wa nyumba ya bibi huyo na kumbaka.
''Bibi alifikishwa kituoni na baada ya uchunguzi wa awali ilbainika ameingiliwa kinguvu na kuachiwa manii sehemu za siri lakini uchunguzi zaidi unaendelea wakati kijana huyu anayetuhumiwa tukimshikilia kwa mahojiano'', amesema Kamanda Moita.
Kamanda ameeleza kuwa baada ya kufanya kitendo hicho cha ubakaji, taarifa za tukio hilo ziliripotiwa katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Rombo na askari kuanza msako mara moja na kufanikiwa kumkamata Daniel.


