Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa vya Maabara
Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.
Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza kujionea huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.
“Mfumo wa malipo ya kielektroniki umeleta ukombozi mkubwa sana kwenye mahospitali nchini. Mapato yameongezeka. Udhibiti wa mapato umekuwa rahisi. Nawaagiza nanyi Hospitali ya Iramba kuhakikisha munafunga mfumo huu wa malipo wa kisasa hususani kwenye: Maabara, Chumba cha upasuaji (Theatre), Dirisha la dawa, na sehemu zote zenye kuingiza mapato”. Ameeleza Dk.Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.
Katika Zahanati ya Kisimba ambayo ipo umbali wa zaidi ya Kilometa 10, Dk. Kigwangalla ameweza kujionea huduma mbalimbali kwenye Zahanati hiyo ambayo ni mpya huku ikiwa msaada mkubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo.