Kufuatia kauli zake za mara kwa mara leo Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jaffo ametumia wasaa wa bunge kumpongeza Mbunge huyo kwa nia yake njema kwa taifa.
''Nimpongeze Mbunge Kessy kwa uhamasishaji wake nchi hii haiwezi kwenda bila bila watu wake kulipa kodi , Ofisi ya Waziri wa fedha Mpango inaendelea na mchakato wa kuhakikisha kila mtu atalipa kodi ili nchi iweze kwenda mbele'' Amesema Naibu Waziri Jaffo.
Aidha Naibu Waziri Jaffo amesema kuwa kila halmashauri nchini zihakikishe kwamba asilimia 5 kwa kinamama na 5 kwa vijana inatoka kutoka katika mapato yao ili vijana hao na kinamama waweze kujiajiri na kuondokana na utegemezi.


