
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.
Jokate amesema watakaobainika kufanya mchezo huo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao bila kujali mamlaka na vyeo walivyo navyo ndani ya chama na Serikali.
Ametoa onyo hilo, wakati akipokea msaada wa magodoro 20 na matenki mawili ya maji yaliyotolewa na wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu na Zainab Vullu kwa ajili ya Shule ya Sekondari Maneromango.
“Tatizo kubwa lipo kwa watendaji na wazazi, sasa nawaambia tumekaa na viongozi wenzangu wa wilaya tumesema hatuko tayari tena kuvumilia suala hili", amesema Jokate.
Kauli hiyo ya Jokate imekuja kufuatia kile alichodai suala la mimba kwa wanafunzi ni changamoto inayoendelea kuitesa wilaya hiyo, huku kiasi kikubwa hali hiyo inachangiwa na wazazi na watendaji wa vijiji pamoja na kata kutotoa ushirikiano ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika na badala yake wanashiriki kupoteza ushahidi.