Thursday , 22nd Oct , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kufungua kongamano la masuala ya kiuchumi pamoja na kutanua sekta mtambuka ikiwemo utawala bora na mawasiliano ya kielektroniki kwa lengo la kukuza a maendeleo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kongamano hilo litawahusisha wataalamu wa masuala ya kiuchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambao watatoa mchango wa mwazo ya kuijenga na kuimarisha uchumi wa sekta ya kilimo, viwanda, elimu, maji na miundombinu.

Akizungumza jijini Dar es salaam mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Prof. Leonard Mwaikambo amesema litafanyika leo na kwamba huu ni wakati muafaka wa mapinduzi ya kiuchumi kutokana na mwelekeo wa taifa.

Prof. Mwaikambo amesema sasa kinachotakiwa kufanyika ni kuwepo kwa uchumi wa ushirikishwaji wa kila mtanzania ili kunufaika na fursa za rasilimali pamoja na huduma zilizoko kwenye maeneo husika kwa mfano mashambani.

Prof. Mwaikambo alisema watanzania wana matumaini makubwa ya kufanikisha malengo ya kufikia uchumi wa kati kutokana na kuwepo kwa fursa nyingi za masoko ya ukanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.