
Jeshi la Polisi Tanzania.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizaya ya Mawasiliano,Sayansi na Tekinologia Selina Lyimo ametoa rai hiyo kwa niaba ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wakati akikabidhi chapisho la utafiti huo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Mbaraka Abdul-Wakil.
Lyimo amesema matokeo ya utafiti huo uliofadhiliwa na wizara hiyo kupitia tume ya Sayansi na Tekinologia COSTECH yana manufaa makubwa katika kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu na kero mbali mbali.
Mtaalamu mwelekezi wa utafiti huo Dakta Haji Semboja amesema utafiti huo umefanyika katika kanda saba na matokeo yameonesha kuwa uhusiano wa kiutendaji baina ya wananchi na jeshi la Polisi umeboreshwa kwa kiwango kikubwa kupitia dhana ya Polisi Jamii.
Dakta Semboja amesema kuwa jambo hilo limesaidia kutengeneza mazingira ya amani na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii zimeendelea kufanyika bila hofu na kwa uhakika wa ulinzi na usalama.