Tuesday , 21st Apr , 2015

Jamii imeshauriwa kuachana na mila potofu za kuwaona watoto wenye ulemavu kama laana kwenye familia zao na kutakiwa washirikiane katika kuwalea ili waweze kutimiza ndoto zao.

Baadhi ya watoto wenye ulemavu wakipokea baiskeli kama msaada.

Wito huo umetolewa jana na mwenyekiti wa baraza la watoto mkoa wa Dodoma, Anna Gelle kwenye mkutano wa baraza la watoto pamoja na viongozi wa serikali kutoka wilaya za Bahi, Chamwino na Manispaa ya Dodoma.

Amesema ulemavu unaweza kumpata mtu yeyote hivyo kuchukulia ulemavu kama laana kwa familia ni kupoteza ndoto za watoto hao ambao wengi wao wana ndoto nzuri maishani mwao lakini zinakatishwa na wazazi.

Kutokana na ripoti ya shivyawata mkoa wa Dodoma, mkoa huu una jumla ya watu wenye ulemavu mbalimbali wapatao 130,400 ambapo walisema idadi hiyo siyo rasmi kutokana na watoto wengi wenye ulemavu kufungiwa majumbani ambao hata hivyo hawajui idadi yao.