Tuesday , 17th May , 2016

Wazazi na walezi mkoani Mtwara, wametakiwa kuacha tabia za kuwafungia watoto nyumbani mwao na kuwanyima fursa ya kwenda shule hasa katika kipindi hiki ambacho serikali inatoa elimu bila malipo kupitia agizo la Rais wa Tanzania, Mhe. John Magufuli.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, akiwa wilayani Tandahimba na kudai kuwa kitendo hicho ni kutomtendea haki rais na watoto ambao wanategemewa kuja kunufaika na uwekezaji unaofanyika mkoani humo hapo baadaye.

Aidha, amesisitiza juu ya utekelezaji wa agizo la rais la kutatua tatizo la uhaba wa madawati nchini kwa kuziagiza wilaya zote mkoani humo kuhakikisha zinatekeleza ipasavyo agizo hilo ambalo mwisho wake ni mwezi Juni mwaka huu.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kwa ushikirikiano wa viongozi na wananchi wa maeneo husika wanaweza kufanya suala la tatizo la ukosefu wa madawati katika mkoa huo kuwa ni historia.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,