Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, John Temu.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, John Temu, amesema jeshi la polisi lilibaini kuwapo kwa watu wanaohisiwa kuwa ni majambazi majira ya saa 3:30 usiku ambao walikusudia kuvamia kituo hicho ambapo polisi walifika eneo la tukio na kuanza kufyatuliana risasi.
Polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema walifika eneo la tukio lakini watuhumiwa hao baada ya kuona gari ya polisi walianza kurusha risasi hovyo ndipo askari walipoanza kujibu mashambulizi na kumpiga risasi mmoja kati ya watuhumiwa hao aliye kuwa na silaha
Katika majibizano ya silaha baina ya polisi na watuhumiwa hao polisi walimpiga mmoja kati ya watuhumiwa hao na ambaye alikimbizwa katika hospitali ya halmashauri ya mji wa makambako ambapo mtuhumiwa alifariki dunia kabla hajafikishwa hospitalini.
Aidha, Temu amebainisha aina ya silaha waliyoikamata kuwa ni Long Life Caliber 22mm yenye namba za usajili A 194300 ambayo ina Darubini ya kuona mbali na kuongeza kuwa silaha hiyo imetengenezwa nchini Czech na ilikutwa ikiwa na risasi tano zilizo kuwa kwenye magazine.