Friday , 31st Oct , 2014

Jeshi la Polisi kikosi cha wanamaji limekamata jahazi moja ambalo linatoka nchini Irani ambalo linadaiwa kuwa na shehena ya dawa za kulevya.

Jeshi la Polisi kikosi cha wanamaji limekamata jahazi moja ambalo linatoka nchini Irani ambalo linadaiwa kuwa na shehena ya dawa za kulevya.

Akizungumza na EATV kamanda wa kikosi hicho Kamanda Mboje Kanga amesema walilikamata jahazi hilo lenye watu ndani, baada ya kulitilia shaka.

Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha kuzuia na kupambana na dawa za kuleya nchini Godfrey Nzowa amesema mapambano bado yanaendelea japo zipo changamoto nyingi na kuongeza kuwa Robo Tatu ya vigogo wa dawa za kulevya wamekwisha kamatwa.