
Naibu Waziri wa Elimu anaeshughulikia Elimu Mh. Kassimu Majaliwa
Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Elimu anaeshughulikia Elimu Mh. Kassimu Majaliwa na kusema kuwa Halmashauri zinazowakata walimu mishahara yao kama kodi za pango za nyumba zilizojengwa na serikali ni makosa Makubwa.
Mh. Majaliwa amesema kuwa lengo la serikali kuzijenga nyumba hizo ni kuwajengea mazingira mazuri ya ufundishaji walimu na kuweza kuwapa urahisi wa kuhudhiria kazini ikiwa ni katika mpango wa kupata matokeo makubwa sasa katika sekta ya Elimu.
Baadhi ya Walimu wamekua wakilalamika kuwa Halmshauri zinawakata mishahara bila ridhaa yao kwa ajili ya kukaa kwenye nyumba za shule ambazo zimejengwa na serikali na kodi zenyewe zinawafanya kushindwa kujiendeleza kiuchumi kutokana na kukatwa kila mwisho wa Mwezi.