Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Inspekta Mkuu wa Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu.
Akizungumza leo katika Shughuli ya uapishwaji wa viongozi wa jeshi la Polisi walioteuliwa hivi karibuni leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, rais Magufuli amesema kuwa taarifa zimezagaa za ubadhirifu wa pesa hivyo wafatilie waweze kuchukua hatua zaidi za kisheria.
Rais Magufuli amesema kuwa jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji fedha ikiwemo kukosa mafuta ya magari, kushindwa kutoa magari yao TRA wakati kunafedha nyingi zimeripotiwa kutumiwa na wajanja wachache.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewaambia jeshi la Polisi kwa kuwa baada ya serikali kufuta maduka ambayo jeshi la polisi lilikua linanunua vifaa na vinywaji kwa bei rahisi sasa fedha hizo ataziongezea kwenye mshahara wao ili wajue kitu cha kufanya kwa kuwa wengi waliokua wanatumia maduka hayo sio polisi.
Aidha Mhe. Magufuli amesema ataliboresha jeshi la Polisi Makazi kwa kujenga nyumba za kutosha ili waweze kufanya kazi kwa weledi na kuwatumikiwa wananchi wa Tanzania kwa utulivu na amani.