Monday , 9th Mar , 2015

Maadhimisho ya siku ya mwanawake dunia yamefanyika jana ambapo inaelezwa kuwa licha ya mafanikioa makubwa yaliyofikiwa swala la elimu kwa mtoto wa kike katika jamii ya kifugaji bado ni tatizo kubwa linalokwamishwa kufikiwa kwa mafanikio.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipongezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Jesca Eriyo.

Hayo yamebainishwa katika makao makuu ya jumuiya ya Afrika mashariki yaliyopo jijini Arusha ambapo yamefanyika maadhimisho hayo kwa nchi za Afrika mashariaki.

Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wamesema kwa sasa wanawake hasa wale waliopo vijijini wameanza kujitokeza katika kugumbea nafasi mbalimbali za uchaguzi huku wengine wakishiriki katika kutoa maoni yao tofauti na ilivyokuwa awali.

Nae mwanasheria anahusika na maswala ya wajane Winfrida Manyanga amesema kwa sasa hali ni mbaya kwa wanawake wa vijiji kwa wanawake wengi kutozifahamu haki zao za msingi tofauti na ilivyo mijini ambapo ametumia maadhimisho haya kuyaomba mashiri mengine kuongeza kuvu katika kuwapatia elimu wanawake wavijiji ili kuzijua haki zao.

Awali adhimisho hayo walitanguliwa na maandamano kutoka makao makuu wa jumuiya na baadae kuelekea katika hospitali ya Mkoa ya mount Meru yakiongozwa na naibu katibu mkuu wa jumuiya EAC Jesca Eriyo na kutoa vifaa mbalimbali katika wodi ya wazazi.