Saturday , 8th Aug , 2015

Mgombea urais kupitia umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Edward Lowasa anatarajia kuchukua fomu siku ya jumatatu katika ofisi za makao makuu ya tume ya taifa ya uchaguzi NEC jijini Dar es salaam.

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa (katikati) akiwa ameshikana mikono na mgombea mwenza, Juma Duni Haji (kushoto)

CHADEMA imeeleza hayo leo jijini Dar es salaam na kutangazwa na Naibu katibu mkuu Zanzibar Salum Mwalimu wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu mpangilio wa shughuli za mgombea huyo kuanza safari ya kusaka urais..

Salumu mwalimu amesema kwa kuzingatia Umoja wao Shughuli hiyo wameamua kuifanyia katika vyama vitatu katika umoja huo ambapo leo wametangazia katika ofisi za NCCR-Mageuzi na keshokwa msafara utakaoanza katika ofisi za CUF Buguruni jijini Dar es salaam hadi NEC na kumalizia ofisi za CHADEMA, Kinondoni.

Mwalimu amesema baada ya zoezi hilo kukamilika jumatatu wataanza kuzunguka na mgombea huyo kumtambulisha kwa wananchi Tanzania Nzima kwa kuwa wanachama na Watanzania walioko mikoani wameonyesha kuwa na hamu ya kumuoa rais wao Mtarajiwa.

Aidha ukawa kupitia kwa Naibu Katibu mkuu mwenza huyo imesema kuwa kujitoa kwa Prof. Ibrahim Lipumba katika nafasi yake ya uongozi kama mwenyekiti wa CUF haiathiri shughuli zozote za UKAWA na wao wanaendelea vyema.