Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba,
Dkt. Tizeba ametoa maamuzi hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia masuala mbalimbali ambapo aliwataja kati ya waliosimamishwa kazi ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula nchini.
Waziri huyo amesema kuwa wakati tahmini ya chakula, nchini haijulikanani kurugenzi ya usalama wa chakula imetoa vibali vya kusafirisha chakula nje bila kufanya tathmini.
Mwingine ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Chakula,(NFRA), Charles Walwa kutokana na kuharibu ghala la chakula na kuisabishia serikali hasara.
Viongozi wa NFRA, Wengine waliosimamishwa ni Mkurugenzi wa uendeshaji wa Huduma Anna Ngoo, Mkurugenzi wa Masoko, Mikalu Mapunda, na Meneja wa NFRA, Songea Jeremia Mtafya.





