Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi amesema kuwa wakati wa kuhitimisha wiki ya elimu mwaka huu kimkoa Aprili 27 mkoa unatarajia kuzindua tuzo ya taaluma ya mkuu wa mkoa ambayo itaambatana na kutoa hamasa kwa wanafunzi, walimu na shule zilizofanya vizuri.
Nchimbi amesema kuwa lengo la tuzo hii ni kuhimiza wanafunzi ambao hawapendi shule kuingizwa shuleni na wanaoishia kidato cha tatu kufika kidato cha nne na ambao hawajaingia kidato cha kwanza kutamani kuingiza ili kupata tuzo hiyo na kuongeza kuwa.
Aidha Nchimbi ameongeza kuwa kuhusu wanaokwamisha wanafunzi wa kike kutimiza malengo yao kwa kuwapa mimba wanao husika na kutafsiri sheria wahakikishe wanafanya kazi yao ipasavyo na watu hao kuogopa kufanya uharibifu huo.
Dkt. Rehema ameongeza kuwa kama wanawake wote wanaoenda shule wangekuwa wanapewa mimba basi serikali isingekuwa na wanawake kwenye ngazi mbalimbali kwa kuwa wangekuwa wameishia njiani.