Monday , 20th Jun , 2016

Takwimu zimeonesha idadi ya wasichana walio katika umri mdogo kati ya miaka 15-19 wanaopata mimba imeongezeka kutoka asilimia 23 mpaka asilimia 27 kutokana na mapungufu yaliyopo kwenye sheria ya ndoa ya mwaka 1971.

Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wa wizara ya afya ,maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt Mpoki Ulisubisya wakati akizindua matokeo muhimu ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto pamoja na malaria na kuongeza kuwa serikali itapambana kwa kila hali kuhakikisha sheria ya ndoa inafanyiwa marekebisho ili waeweze kukabiliana na tatizo la mimba za utotoni.

Aidha akizungumzia utafiti kuhusu ugonjwa wa malaria amesema kuwa utafiti unmebaini kuwa matumizi ya vyandarua yamepungua sana kutokana na wananchi kuamua kutumia vyandarua hivyo kwa matumizi mengine ikiwemo ni pamoja na kiutumia kama uzio, vifaa vya kuvulia na wengine kutumia kama vazi.