
Dalili za ukoma
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu, imezitaja halmashauri za wilaya zinazoongoza katika mikoa hiyo kuwa ni Lindi (Lindi Manispaa, Liwale, Lindi na Ruangwa), Morogoro (Halmashauri ya Ulanga, Kilombero na Mvomero), Dar es Salaam (Manispaa ya Temeke na Kigamboni), Tanga ( Halmashauri za Muheza, Mkinga na Pangani),
Nyingine ni Mtwara (Halmashauri ya Nanyumbu na Newala), Rukwa (Halmashauri ya Nkasi), Pwani (Halmashauri ya Rufiji na Mkuranga), Geita (Halmashauri ya mji Geita na Halmashauri ya Chato), Tabora (Halmashauri ya Sikonge), Mwanza (Halmashauri ya Kwimba na Misungwi), na Ruvuma (Halmashauri ya Songea na Namtumbo).
Takwimu zinatuonyesha kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kutokomeza ugonjwa huu kutoka kiwango cha utokomezaji cha watu 0.9 kati ya watu 10,000 mwaka 2006 na kufikia kiwango cha watu 0.4 kati ya watu 10,000 mwaka 2015 wakati kiwango cha kimataifa cha utokomezaji ukoma kinatakiwa kuwa chini ya mgonjwa 1 katika watu 10,000.
Waziri Ummy Mwalimu
Amesema katika miaka 10 iliyopita, ugonjwa wa ukoma peke yake umeongeza idadi ya watu wenye ulemavu wa kudumu zaidi ya 2,800 hapa nchini na kwa mwaka 2015 pekee walemavu wapya wapatao 300 waligunduliwa miongoni mwa wagonjwa wapya wa ukoma, kati ya hao watoto walikuwa 26
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Tuepuke ulemavu unaotokana na ukoma miongoni mwa watoto”.
Waziri Ummy pia amesema kuwa ugonjwa huo unatibika na kupona kabisa. na endapo mgonjwa akijitokeza na kugunduliwa mapema hupona vizuri bila madhara yoyote.
Ukoma huenezwa kwa njia ya hewa toka kwa mtu anayeugua na ambaye hajaanza matibabu. Dalili za ukoma ni pamoja na baka au mabaka yenye rangi ya shaba mwilini. Mabaka haya hayaumi wala hayawashi bali hupoteza hisia unapoyagusa na yanaweza kujitokeza mahala popote mwilini, kuanzia kichwani hadi miguuni.
“Siku ya Ukoma Duniani” huadhimishwa kila mwaka, Jumapili ya mwisho wa mwezi Januari.
Siku hii iliasisiwa na mwandishi wa habari mfaransa, Raoul Follereau aliyetumia muda wake mwingi kuzunguka dunia kueleza hali duni ya maisha ya watu walioathirika na ugonjwa wa ukoma.
Raoul Follereau