
Picha ya moto
Mkuu wa Upelelezi kanda hiyo, Camillius Wambura amesema wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano na kwamba polisi wamekwenda kwenye maeneo ambayo mtuhumiwa aliyataja kufanyia mauaji na wamechukua majivu kwa ajili ya vipimo vya DNA ili kupata uthibitisho.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa kuwa Luwoga na mke wake Naomi hawakuwa na maelewano ya muda mrefu.
Naomi alitoweka nyumbani kwake Mei 15, 2019, ambapo familia yake ilitoa taarifa za kutoweka kwake katika kituo cha Polisi Chang'ombe, baada ya Luwoga kuwapa taarifa siku nne baada ya Naomi kutoonekana nyumbani.