Saturday , 23rd Jul , 2016

Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic Hillary Clinton amemteuwa Seneta Tim Kaine, kutoka Virginia kuwa mgombea wake mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini humo tarehe 8 Novemba.

Bi Hillary Clinton (Kushoto) akiwa na Tim Kaine

Bi Clinton alitangaza uteuzi huo kupitia akaunti yake ya Twitter akimtaja mgombea mwenza huyo kuwa ni mfuasi mkubwa wa makubaliano huru ya biashara na anatarajia kumtambulisha rasmi leo katika mkutano wa hadhara huko Miami.

Kaine ambaye anaongea kihispania vizuri anatarajia kuwavutia wapiga kura wamarekani wenye asili ya Uhispania kundi ambalo ni kubwa katika chaguzi za Marekani.