Wednesday , 6th May , 2015

Ofisi ya madini wilaya ya Chunya mkoani Mbeya imekusanya mrabaha wa sh. Milioni 719.7 kutokana na dhahabu iliyozalishwa wilayani humo katika kipindi cha Julai mwaka 2014 hadi April mwaka huu.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage.

Hayo yamesemwa na ofisa madini wa wilaya hiyo Ronaldo Mremi wakati akitoa taarifa kwa naibu waziri wa nishati na madini, Charles Mwijage alipokuwa akikagua miradi ya umeme ya awamu ya awamu ya pili.

Mremi amesema katika kipindi hicho ofisi hiyo pia imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh. Milioni 187.6 ikiwa ni mikusanyiko inatokana na ada ikiwamo ada ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini na kodi ya mwaka kwa wamiliki wa leseni.

Kwa upande wake Mwijage aliwataka watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kufikia malengo yaliyowekwa na wizara hiyo.