
Akiongea na East Africa Radio jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa CHODAU mkoa wa Kinondoni Bw. John Msele amesema uwepo wa taarifa hizo itawawezesha waajiri kuepuka baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu ambao wanaweza kufanya uhalifu wa aina mbalimbali ikiwemo kuiba mali, mtoto au kutekeleza mauaji.
Bw. Masele amesema ni vyema wenyeviti wa serikali za mitaa wa wilaya hiyo kuhakikisha kuwa wanakuwa na taarifa za wahudumu wa majumbani katika mitaa yao jambo ambalo litawasaidia katika kupigania, kutetea na kulinda haki na sheria za wahudumu wa ndani sambamba na kulinda haki za waajiri wao.
Aidha, Masele amekemea tabia ya baadhi ya waajiri kuwalipa wafanyakazi chini ya kiwango cha serikali, malimbikizo ya muda mrefu, kuwanyima likizo za uzazi pamoja na kuwafundisha wafanyakazi wao kusema kuwa wapo kwa ndugu zao kuacha mara moja kwani wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.