Friday , 22nd Apr , 2016

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema hakijaridhishwa na uamuzi wa rais Dkt. John Magufuli kumsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe huku aliyekuwa Meya Jiji Didas Masaburi akiachwa.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Dar es salaam, Benard Mwakyembe akizungumza na waandishi

Wakiongea Jijini Dar es Salaam, Viongozi wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ,Mkoa wa Dar es Salaam, Bernad Mwakyembe na Katibu wake Henri Kileo , wamesema kuwa utumbuaji majibu wa rais ni kama kiini macho kwa sababu hakuna mabadiliko yoyote kwa wananchi wa Tanzania.

Aidha wametaka hatua stahiki zichukuliwe ikiwemo pamoja na kupelekwa mahakamani kwa wanaohusishwa na ubadhilifu huo ili hatua zaidi zichukuliwe ikiwemo na kurudishiwa fedha za wananchi walizozitafuta.

Aidha wameongeza kuwa Utenguzi wa Aliekuwa Mkurugenzi wa Jiji ungesubiri kikao cha baraza la madiwani ambacho kingefanyika na si vinginevyo na kuongeza kuwa rais angekuwa anawapa muda wa kujieleza wale wote wanaotumbuliwa.

Aidha viongozi hao wamesema kuwa rais anaonyesha kutumbua majipu lakini anaowatumbua sio wahusika wakuu wa ubadhirifu huo na kumtaka rais awatumbue na wale ambao wako nyuma ya pazia katika ufisadi huo.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho , mkoa wa Dar es Salaam, Bernad Mwakyembe na Katibu wake Henri Kileo , wakizungumzia kutoridhishwa kwao