Friday , 14th Aug , 2015

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, amewataka wananchi mkoani hapa, kujitokeza kwa wingi jumamosi, kumdhamini Mgombea uras kwa tiketi ya Chama hicho, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Mgombea uras kwa tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Lowassa atawasili mkoani Arusha akitokea uwanja wa Ndege wa kimataifa (KIA), hadi viwanja vya Tindigani Kimandolu atakapokuwa na mkutano wa hadhara.

Aidha mapokezi hayo yatakuwa makubwa na ya historia, yataambatana na ngoma za kila aina ya makabila nchini watakaokuwa wakitumbuiza kuanzia anashuka uwanjani hadi atakapokutana na wadhamini, kisha ataelekea Wilayani Monduli atakakokuwa na mkutano wa hadhara pia.

Akizungumza na waandishi wa habari,kwenye ofisi za Chadema Mkoa, akiwa ameambatana na Viongozi wa Chama cha wananchi CUF wa Mkoa huo, Golugwa
amesema Lowassa anatarajiwa kushuka KIA majaira ya saa 3 tatu asubuhi na atakuwa ameongozana na viongozi wa Kitaifa wa Umoja wa Wananchi UKAWA.

Amesema wanatarajia kuwa na magari 75 yatakayobeba wafuasi wa Ukawa watakaopenda kwenda KIA kushuhudia historia ya aina yake ambayo yatondoka ofisi za Chadema Mkoa saa mbili asubuhi.

Pia amesema katika mkutano huo wanatarajia viongozi mbalimbali wa CCM wakiwemo wenyeviti wa serikali za mitaa, mabalozi na vigogo wengine watapokelewa rasmi katika mkutano huo wa hadhara.

Amesema kuhusu hali ya usalama ipo vizuri na watakuwa na ulinzi wa Polisi kwa kushirikiana na walinzi wa chama hicho ili kuhakikisha usalama na amani unatawala kwa kuw ana magri matano maalum ya wagonjwa.

Golugwa amesema pia kuna mmoja wa wafuasi amejitolea gari lake la kukusanyia takataka litakalopambwa kwa nembo za Chama na mgombea Urais wa UKAWA ambalo litatumika kutupia kadi za CCM ambazo wanatarajia zitakuwa nyingi kupitiliza.

Naye Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini, Derick Magoma, amesema kuwa kuanzia kesho, litapita gari maaluma la aina yake ambalo halipo Tanzania, lenye mziki mkubwa, sehemu ya kupumizikia na jukwaa, litaanza kupita mtaanai kutangaza ujuio wa Mheshimiwa Lowassa.