Wednesday , 23rd Mar , 2016

Mchakato wa kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa 2,000 umeshaanza ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari viwili nchini humo kuruhusiwa kurusha upya matangazo nchini Burundi.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Alain Aimé Nyamitwe

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Alain Aimé Nyamitwe amesema hayo nje ya Mkutano wa Baraza la USalama la Umoja wa Mataifa kwenye mjadala maalum uliofanyika kuhusu usalama kwenye ukanda wa Maziwa Makuu.

Aidha ametangaza kwamba maafisa 200 kutoka Muungano wa Afrika watapelekwa nchini Burundi kuchunguza hali ya haki za binadamu na utaratibu wa kusalimisha silaha, baada ya mradi wa kupeleka ujumbe wa ulinzi wa Amani MAPROBU kusitishwa.

Halikadhalika amethibitisha kwamba utaratibu wa kuanzisha ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi unaendelea, zikitarajiwa kufunguliwa baada ya miezi michache, na akiutaka Umoja wa Mataifa uangazie hasa masuala ya uwekezaji na ajira kwa vijana.