Tuesday , 28th Jun , 2016

Diwani wa kata ya Mabibo Kasim Lema amesema kuwa mpango wa Bunge la Jamii unaoendelea katika Kata hiyo umesaidia sana katika kupunguza matatizo yaliyokuwa yanawakabili wakazi wa eneo hilo kwani kwa hivi sasa wanauwezo wa kukutana na kujadili pamoja.

Bw Lema ametoa kauli hayo alipokuwa kiongea wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kujadili mafanikio yaliyofikiwa na bunge hilo liloloratibiwa na mtandao wa kijinsia TGNP na kubainisha kuwa unapohusisha jamii katika kujadili matatizo yanayowakabili wao wenyewe inakuwa ni rahisi zaidi katika kupatikana ufumbuzi zaidi ya mtu mwingine akijitokeza kutatua matatizo yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti bunge la jamii Kipunguni Selemani Bishagazi amesema kuwa bunge la jamii limewawezesha kugundua kuwa katika mitaa yao kulikuwa na gesti bubu ambazo zilikuwa zinatumika na vijana wa kiume kuwarubuni watoto wa kike na kusababisha mimba za utotoni hivyo wamefanikiwa kufunga gesti hizo 7 ili kuwanusuru watoto wa kike.