Thursday , 25th Sep , 2014

Baraza la wanawake la Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA nchini Tanzania BAWACHA limeandaa maandamano kwa wanawake ambayo yanalenga kumuomba Rais Jakaya Kikwete kutosaini rasimu ya katiba kwa madai kwamba itakuwa haijapatikana kama wananchi wa

Mwenyekiti wa BAWACHA na Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee

Mwenyekiti wa BAWACHA na Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee amesema maandamano hayo yatafanyika baada ya wiki moja kuanzia sasa na kwamba yanalenga kuhakikisha rasimu hiyo ya katiba inapatikana kwa kutokana na michango ya mawazo kwa pande zote na vyama vyote vilivyopo kisheria.

Mdee amesema maandamano hayo hayatahusisha wanawake wa chama hicho pekee bali yatahusisha pia wanawake kutoka maeneo yote ya jiji kwa lengo la kufikisha ujumbe husika .