
Magari yakipita kwenye barabara za juu
Msemaji mkuu wa serikali Dkt. Abbas Hassan, amethibitisha kuwa kuanzia leo serikali imeruhusu rasmi matumizi ya barabara hizo hadi pale uzinduzi utakapofanyika mwezi ujao.
Naweza kuwathibitishia kuwa leo Serikali imeamua rasmi kuruhusu magari kutumia daraja la juu la Tazara kuelekea uzinduzi rasmi utakaofanyika mwezi ujao.
Tunaahidi, tunatekeleza.
Dkt. H.A pic.twitter.com/hcIjJbr8qG
— Msemaji Mkuu wa Serikali (@TZMsemajiMkuu) September 15, 2018
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea barabara hizo za juu tarehe 29/8/2018, katika makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere (Tazara) na kusema mradi huo umekamilika kwa asilimia 98.
Katika ziara yake hiyo Majaliwa aliweka wazi kuwa wakati wowote kuanzia Oktoba, 2018, Rais John Magufuli atazindua barabara hiyo ambayo imepewa jina la Mhandisi Patrick Mfugale.
Serikali ya Tanzania ilisaini mkataba wa ujenzi wa barabara hizo na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction ya Japan mwaka 2015 na kueleza kuwa mradi huo utagharimu zaidi ya Sh87 bilioni.