Mtu huyo aliyepigwa na marungu, alifanya kitendo hicho kipindi cha sikukuu ya Eid.
Taarifa ya tukio hilo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi wakati akizungumza na East Africa Radio kuhusu matukio yaliyojitokeza kipindi cha sikukuu ya Eid na sikukuu ya Sabasaba, na kusema tukio hilo limetokea baada ya mtu aliyeibiwa kuku hao kuomba msaada kwa wananchi na wananchi kumkamata mwizi huyo na kuanza kumpiga na silaha hizo mpaka kumsababishia mauti.
Kamanda Msangi amesema jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia watu watatu kwaajili ya mahojiano ya tukio hilo na kuwataka watanzania kuacha kufanya vitendo vya kiarifu kwa kisingizio cha kukosa ajira za kuwaingizia kipato cha kila siku, kwani vitendo hivyo vya kiharifu vinagharimu maisha yao na kuwasababishia kifo.
Amewaasa watanzania kuacha kujichukulia sheria mkononi na watumie vyombo vya usalama katika kupambana na wahalifu.



