Tuesday , 19th Dec , 2017

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis anayekabiliwa na shtaka la rushwa ameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma na kuoewa masharti ya kutotoka nje ya Tanzania bila kibali  cha mahakama.

Sadifa ambaye alifikishwa mahakamani leo Disemba 19, baada ya kukosa dhamana wiki iliyopita kutokana na upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kiapo kuzuia dhamana kwa madai kuwa angevuruga upelelezi na kuingilia uchaguzi wa UVCCM uliofanyika mjini Dodoma.

Mahakama leo imetupilia mbali pingamizi hilo na kutoa masharti ya dhamana kwamba Sadifa awe na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh1 milioni na wenye vitambulisho vinavyotambuliwa na mamlaka ya maeneo wanakoishi.

Aliyekuwa Mwenyekiti UVCCM Sadifa  Juma Khamis

Sadifa pia ametakiwa kutotoka nje ya mipaka ya nchi bila kibali cha Mahakama. Amekidhi masharti hayo na amechiwa kwa dhamana na kesi itatajwa Januari 18,2018.

Kiongozi huyo alikuwa akituhumiwa kwa kitendo cha kuwahonga wanachama na shtaka la pili ni kuwaahidi kuwalipia usafiri wanachama wa umoja huo kuwasafirisha kutoka Dodoma hadi Kagera kama zawadi ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi mkuu wa umoja huo Disemba 9