Bibi Scholarstika Mhagama pembeni ya jeneza alilotengeneza miaka 2o iliyopita
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Sholastika Mhagama mwenye umri wa miaka 76 ambaye nimlemavu wa miguu mkazi wa kijiji cha Lundusi kata ya Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma amejichongea jeneza analokaa nalo kwenye nyumba yake kwa madai ya kutengwa na ndugu zake kutokana na ulemavu wake pamoja na kuchoshwa na shida za dunia.
Hotmix imefunga safari hadi Peramiho na kumfuata mwanamke huyo aliyepata ulemavu akiwa darasa la pili baada ya kuumwa na nyoka hali iliyosababisha kukatwa mguu mmoja.
Mwanamke huyo ambaye pia alifiwa na mumewe na wanae wanne, amesema jeneza hilo alilitengeneza kwa miaka zaidi ya ishirini iliyopita kwa pesa ya kuuza pombe miaka.
Tukio lingine kutokea Songea ni kwamba Siku moja baada ya jengo moja la ghorofa kuungua moto mjini songea mkoani Ruvuma watu wawili wamejeruhiwa katika ajali nyingine ya moto iliyotokea maeneo ya Mfranyaki baada ya nyumba moja mali ya Khalifa Omary kuungua moto na samani zote za ndani kuteketea.
Vilio na majonzi vilitawala eneo la tukio ambapo majeruhi wawili waliojeruhiwa katika ajali hiyo ambao ni Cauthery Namahala binti wa miaka kumi na moja na Maria Shaweji binti wa miaka kumi na tano ambao walizimia kutokana na moshi wa moto na kukimbizwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.
Tukio hilo la ajali ya moto limetokea ikiwa imepita siku moja baada ya jengo moja la ghorofa lililoko katikati ya mji wa Songea kuungua moto.