Tuesday , 25th Nov , 2014

Watu 8 wamefariki dunia na wengine 10 kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Hiace kutoka mjini Kahama kuelekea mjini Shinyanga kupinduka katika eneo la Buhangija Kona kwenye barabara kuu ya lami ya Tinde – Shinyanga.

Mashuhuda wa ajali hiyo na majeruhi wamesema imetokea muda wa saa 4.30 Asubuhi wakati dereva wa gari hilo la abiria lenye namba za usajili T 761 CKB aliyefahamika kwa jina la Annuar Awadh aliyeruka kwenye gari kabla ya ajali hiyo na kutokomea kusikojulikana aliporuka tuta la barabarani akiwa mwendo kasi na kusababisha gari hilo kupoteza mwelekeo na hivyo kuingia kwenye mtaro mkubwa kando ya barabara na kupinduka.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya serikali ya mkoa wa Shinyanga Dkt. Mfaume Salum amesema hospitali yake imepokea marehemu watano waliofia eneo la ajali na majeruhi kumi na watatu ambapo wengine watatu wamefariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo wakiwa wanapewa matibabu.

Hata hivyo kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Bw. Longnus Tibishubwamo ambaye alikuwepo eneo la tukio hakuwa tayari kuzungumza na waandishi wa habari kwa madai kuwa yeye si msemaji wa jeshi hilo.