Tuesday , 4th Aug , 2015

Imeelezwa kuwa ajali nyingi zinazotokea ni kutokana na vyanzo vya ajali ambavyo vinaweza kuzuilika ikiwemo uendeshaji wa gari kwa mwendo kasi, ukosefu wa umakini barabarani pamoja na kuendesha magari mabovu barabarani.

Rais Jakaya Kikwete Awaaga Wananchi wa Tanga.

Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo kitaifa imefanyika mkoani Tanga.

Rais Kikwete amesema tafiti zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinazotokea barabarani ni kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika pindi sheria za usalama barabarani zitakapofuatwa na kuacha uzembe

Kwa upandea wake mwenyeji wa maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Tanga Magalula Said Magalula amesema kwa mujibu wa takwimu za ajali kutoka kikosi cha usalama barabarani zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2012 mkoa wa Tanga umekua wa tano bora katika mikoa iliyopunguza ajali za barabarani nchini.

Nae kamanda wa kikosi cha usalama barabarani taifa Mohamed Mpinga ameeleza kuwa lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuwakumbusha na kuwaelimisha watumiaji wote wa barabara jinsi ya kuzitumia barabara kwa usalama zaidi pamoja na kujua madhara yanayoweza kutokana na ajali zinazoweza kutokea.

Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yamefanyika mkoani Tanga ikiwa ni maadhimisho ya tatu kitaifa kufanyika mkoani hapa ikiwa kauli mbiu ya mwaka huu ikisema ENDESHA SALAMA OKOA MAISHA.