Friday , 15th Jul , 2016

Wahudumu wa sekta mbalimbali za kijamii Mkoani Tabora na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ilolangulu mkoani humo wameanza kunufaika na mpango wa kuunganishwa na kujifunza kupitia wa mtandao wa Airtel kwa huduma za Internet ya bila malipo.

Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Wahudumu hao kutoka sekta za Elimu, Afya, Maji na Kilimo wamesema kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel imewawezesha kuwa na mawasiliano ya karibu na Jamii wanayoihudumia na kuweza kukusanya takwimu za kila mwezi kwa njia ya mtandao. Na kuwezesha utekelezaji wa kazi zao kuwa wa uhakika kutokana na kuwafikia wanufaika kwa urahisi

Baadhi ya Wanafunzi walionufaika na kuunganishwa na huduma ya mafunzo kwa mtandao wamesema wanafanya vizuri katika masomo yao na kufaulu kupitia huduma hiyo

Ayub Kim kutoka mradi wa Mileniam Promise Tanzania amesema mtandao wa Airtel umewawezesha Walimu na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ilolangulu kupata taarifa za kimtandao na zinasaidia kuinua kiwango cha elimu.

Uongozi wa shule hiyo umesema kupitia mtandao huo Wanafunzi sasa wan auwezo wa kupata taarifa mbali mbali za kimasomo kutoka ndani na nje ya nchi na hivyo kuongeza kiwango cha ufaulu.

Mpango wa kutoa laini za simu zisizona malipo umebuniwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa la kurahisisha taarifa za kimtandao kwa watoa huduma waishio vijijini