Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro,
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro, amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu wote watakaokaidi kujitokeza katika uhakiki huo wa Silaha.
Wakatia huohuo Kamishana Siro amewaonya watu wanaotumia vibaya majina ya viongozi kutapeli kwa ajili ya kujipatia fedha au huduma kutoka katika taasisi au mtu yoyote.
Kamishna Sirro amesema kuwa polisi inawasaka na itawachukulia hatua wenye tabia hiyo kwa kuwa ni matapeli huku akiwataka watanzania kuwa makini na simu wanazopigiwa kupewa taarifa za masuala yanayohusiana na pesa.
Kamishna Sirro ametoa Onyo hilo siku moja baada ya watu wanne kupandishwa kizimbani katika mahakama ya kisutu kwa tuhuma za kujitambulisha kwa kutumia jina la Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.
Kamishna Sirro amesema mtu anapokuwa na Mashaka na kitu chochote ate taarifa polisi mara moja kama alivyofanya mkurugenzi wa kampuni ya Usangu Ligistics baada ya kupokea simu kutoka mtu aliejitambulisha kwa jina la waziri Mkuu.