PAZIA VPL LAFUNGWA, AZAM KUKABIDHIWA KOMBE CHAMAZI
Michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara inafikia tamati kesho (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku mabingwa wapya Azam wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.