Picha ya msanii Mo Music
Akipiga stori na eNewz ya East Africa TV, Mo Music amesema ameshakuwa staa na mtu mkubwa hivyo hawezi kushuka kimuziki.
"Tayari nimeshaacha alama na sijawahi kushuka kimuziki, mpaka Dunia inapinduka hakutakuwa na Mo Music mwingine, halafu mimi napenda kuringa na hakuna kitu kizuri kama shabiki anakuuliza kwanini haurudi, kwahiyo wanakuwa wanakumiss na una nafasi yako" ameeleza Mo Music.
Pia ameendelea kusema kwa mwaka 2019 hakufanya chochote cha maana kwenye muziki kwa sababu alikuwa bize na biashara zake zingine, ambazo zilikuwa zinamsaidia kumuingizia pesa.

