Alhamisi , 22nd Sep , 2022

Vilabu 20 kutoka mikoa 7 vinaendelea kuchuana vikali kugombania Taji la Ligi ya Taifa ya mchezo wa mpira wa Wavu 2022 inayoendelea kushika kasi kwenye uwanja wa ndani wa Taifa huku michezo ya mzunguko wa pili ikitaraji kuhitimishwa Septemba 24, 2022 jijini Dar es Salaam.

Naibu katibu Mkuu wa chama cha mpira wa wavu Tanzania (TAVA) Shukuru Ally amesema michezo ya mzunguko wa pili kwa upande wa Wanaume na Wanawake inataraji kuhitimishwa jumamosi ya wiki hii huku washindi wawili wa kila kundi watafuzu kushiriki hatua ya michezo ya Play Off .

"Mzunguko wa tatu ambao kutakuwa na mchezo wa mtoano utapigwa mwezi ujao pamoja na fainali ili tupate mshindi wa jumla'' Amesema Ally.

Kwa upande wao wachezaji wanaoshiriki mashindano hayo wamewapongeza TAVA kwa kurudisha ligi hiyo ambayo itachochea ushindani kwa vilabu na kuhamasisha watu wengi kujitokeza kucheza mchezo huo