Jumanne , 24th Mei , 2022

Nyota wa mpira wa miguu wa West Ham, Kurt Zouma amekiri mashtaka yake mahakamani alimpiga teke na kibao paka wake mwezi Februari mwaka huu.

Zouma mahakamani leo.

Februari mwaka huu ilisambaa video ya Zouma akimpiga paka, video hiyo iliwekwa katika mitandao ya kijamii na mdogo wake Yoan.

Zouma amekiri alitenda makosa kwa kuvunja sheria ya ustawi wa wanyama. Kesi yake itasikilizwa tena Juni 1 mwaka huu. Paka wake alichukuliwa na Jumuiya ya Kifalme ya Kuzuia Ukatili (RSPCA) na anatafutiwa makazi mapya.