Yanga yapingwa Chamanzi

Saturday , 12th Aug , 2017

Klabu ya Yanga imelazwa leo kwa goli moja kwa sifuri dhidi ya klabu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Chamanzi jijini Dar es Slaaam 

Kikosi cha Yanga

Goli la Ruvu Shooting limepatikana katika dakika ya 21 ya mchezo baada ya beki mpya wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' kujifunga kwa kichwa wakati akiokoa mpira ambao ulikuwa unaelekea wavuni na kupelekea Ruvu Shooting kushinda goli la kuongoza lililodumu mpaka dakika za mwisho za mchezo.

Kwa upande Nahodha wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' ameipongeza klabu ya Ruvu Shooting kwa kupata ushindi huo na kusema kuwa klabu yao bado inajipanga kwani imesajili wachezaji wengi na kusema kuwa bado wachezaji miili yao haijafunguka vizuri kutokana na mazoezi ya muda mrefu ya kujenga miili, hivyo amedai mwalimu bado anaendelea kuona mapungufu na kukipanga kikosi zaidi. 

Klabu ya Ruvu Shooting imevunja historia na kuandika historia ya kuifunga klabu ya Yanga kwani haijawahi kushinda katika mechi yoyote dhidi ya Yanga. Klabu ya Yanga kesho pia inatarajiwa kushuka dimbani Zanzibar dhidi ya Mlandege FC katika mchezo wa kirafiki.