Jumatatu , 24th Jan , 2022

Ligi Kuu soka Tanzania bara ikiwa inaendelea kushika kasi tukiwa raundi ya 13, mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora nazo zinaendela, mshambuliaji wa Namungo FC Reliant Lusajo ndio kinara wa ufungwa akiwa na mabao 7 na Yanga ndio timu iliyofunga mabao mengi 23 mpaka sasa.

Reliant Lusajo kulia ana mabao 7 ndio kinara wa ufunga, akifuatiwa na Fiston Mayele kushoto mwenye mabao 6.

Mpaka sasa kwenye Ligi kuu NBC Premier League yamefungwa jumla ya mabao 197 katika michezo 103 iliyochezwa, ukiwa ni wastani wa bao 1.0097 linafungwa kwa mchezo na vinara wa Ligi klabu ya Yanga ndio timu iliyofunga mabao mengi mabao 23 na Mtibwa Sugar ndio timu iliyofunga mabao machache zaidi mabao 7.

Kwenye vita ya ufungaji mshambuliaji wa Namungo FC Reliant Lusajo ndio kinara amefunga jumla ya mabao 7 akifuatiwa na Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 6, George Mpole wa Geita Gold, Jeremia Juma wa Tanzania Prisons na Vitalis Mayanga wa Polisi Tanzania wote wamefunga mabao 5.

Huku Feisal Salum, Saido Ntibanzokiza waote wa Yanga wamefunga mabao 4, wachezaji wengine waliofunga mabao 4 ni Meddie Kagere wa Simba, Juma Luzio na Richardson Ng'odya wote wa Mbeya City. Mpaka sasa wachezaji wazawa (watanzania) wametawala kwenye orodha ya wachezaji 10 waliofunga mabao mengi wapo 7 wachezaji wa kigeni ni 3 tu.

Msimu uliopita mfungaji bora wa Ligi alikuwa John Bocco wa Simba SC ambaye alimaliza msimu akiwa na bao 16, Lakini mpaka sasa msimu huu bado hajafunga bao hata 1. Na imesalia michezo 17 kabla ya kuumaliza msimu huu wa 2021-22.