Jumanne , 17th Mei , 2022

Nahodha wa klabu ya Arsenal Granit Xhaka amewajia juu wachezaji wa kikosi hicho baada ya kufungwa na Newcastle United mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Akiwataka wachezaji ambao hawapo tayari kujitoa kuipambania klabu wabaki nyumbani au wasicheze kabisa.

Arsenal wamefungwa michezo miwili mfululizo na kupoteza matumaini ya kucheza Ligi ya mabingwa msimu ujao

Xhaka hajapendendwa na kiwango cha uchezaji kilichoonyeshwa na baadhi ya wachezaji wenzake kwenye mchezo huo ambao ulikuwa ni muhimu kwao kushinda ili kufufua matumaini yakufuzu Ligi ya mabingwa Barani ulaya kwa mara ya kwanza baada ya misimu 5.

"Kama mtu hayuko tayari kucheza mchezo huu, akae nyumbani, haijalishi umri wako. Ukiwa na woga, kaa benchi au ubaki nyumbani, unahitaji watu waje kucheza mpira. Ni moja ya michezo muhimu sana kwetu. Tumewaangusha sana watu waliokuja hapa. Amesema Xhaka

Kipigo hicho kimeiweka The Gunnars kwenye mazingira magumu ya kufuzu kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao kutoka na kipigo hicho ambacho kimewafanya wasalie nafasi ya 5 kwenye msimamo wa EPL wakiwa na alama 66 tofauti ya alama 2 dhidi ya Tottenham wenye alama 68 wakiwa nafasi ya 4 na umebaki mchezo mmoja kabla ya Ligi kumalizika.

Kwa matokeo hayo ili Arsenal iweze kufuzu kucheza Champions league msimu ujao inabidi washinde mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya Everton lakini pia Tottenham wafungwe na Norwich City ili wao waweze kumaliza katika nafasi ya 4. Katika ushindi huo wa Newcastle bao la kwanza beki wa Arsenal Ben White alijifunga na Bruno Guimares alifunga bao la Pili.