
Mchezaji wa kimataifa wa Zambia, Rainford Kalaba, alifunga mabao mawili, katika mchezo huo, ambao, ulikuwa wa marudiano baada ya kutoka 1-1 wiki iliyopita, mjini Blida.
Mazembe imeshinda kwa jumla ya mabao 5-2, na hili ni taji lao la pili mfululizo katika mashindano ya Afrika, baada ya mwaka uliopita kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa.