Simba SC, Yanga SC, Azam FC
Jumla ya timu nane zimefuzu katika hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo, ambazo ni Simba SC, Yanga SC, Kagera Sugar, Alliance FC, Azam FC, Namungo FC, Sahare All Stars na Ndanda FC.
Katika timu hizo zilizofuzu, timu pekee iliyofuzu nje ya timu za Ligi Kuu ni Sahare All Stars kutoka Tanga ambayo ni timu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza katika kundi B, ambapo inakamata nafasi ya nane katika kundi lake.
Wakati droo ya hatua ya Robo Fainali ikisubiriwa kupangwa, mashabiki wa soka hasa wa klabu hasimu za Simba na Yanga wameonesha shauku ya kutaka timu zao zipangwe katika hatua hiyo ili waoneshane umwamba.
Timu hizo zitakutana katika ligi, Machi 8, 2020 katika mchezo wa pili, baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, Januari 4.

