Jumamosi , 26th Mei , 2018

Baada ya kuonesha kiwango kikubwa kwenye ligi kuu msimu huu, mshambuliaji wa Lipuli FC Adam Salamba, amekuwa akiwaniwa na timu kubwa za ligi kuu zikiwemo Yanga, Simba na Azam FC. 

Tetesi kutoka ndani ya klabu ya Lipuli FC tulizozipata jioni hii zinasema timu hiyo pamoja na mchezaji wamepokea ofa nono kutoka Simba, hivyo nyota huyo anaelekea Msimbazi kwaajili ya msimu ujao.

Chanzo chetu kimeeleza kuwa Salamba na Lipuli FC wamekubali ofa ya zaidi ya milioni 80, zikiwemo gharama za ada ya uhamisho pamoja na pesa ya mchezaji mwenyewe.

Aidha chanzo hicho kimeeleza kuwa Simba imevizidi vilabu vya Azam FC na Yanga kwenye dau ambalo wameweka mezani huku mchezaji mwenyewe akivutiwa kwenda Simba kutokana na ofa yao kujumuisha vitu vya ziada kama mchezaji kupewa usafiri.

Salamba ndio alikuwa mwiba kwenye mechi ya raundi ya pili ligi kuu soka Tanzania Bara iliyopigwa uwanja wa Samora mjini Iringa na timu hizo kutoka sare ya 1-1 na Salamba akiwa ndio mfungaji wa bao la Lipuli FC.