Alhamisi , 23rd Jun , 2022

Taarifa za usajili barani Ulaya leo Alhamisi Juni 23, 2022. Miongoni mwa taarifa Ousmane Dembela anataka kubaki Barcelona, PSG wanampango wakumfuta kazi Pochettino na Neymar huwenda akuuzwa ikija offa nzuri.

Neymar Jr ana umri wa miaka 30

Winga wa FC Barcelona Ousmane Dembele amemwambia kocha mkuu wa klabu hiyo Xavi Hernandez kuwa anataka kubaki Barcelona. Mkataba wa Dembele na Barcelona unamalizika mwishoni mwa mwezi huu Juni 2022. Winga huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 anahusishwa kujiunga na Chelsea ya England. Kama hata ongeza mkataba mpya ataondoka akiwa mchezaji huru.

kocha wa Nice Christopher Galtier amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya PSG kwa mkataba wa miaka miwili (2). Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Ufaransa zinaripoti kuwa kocha Galtier amefikia makubaliano na viongozi wa PSG kuja kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua mikoba ya Mauricio Pochettino anayetarajiwa kufutwa kazi.

Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi alidhibitisha kuwa wapo kwenye mazungumzo na kocha huyo. PSG inampango wa kumfuta kazi Pochettino baada ya kushindwa kukiongoza kikosi hicho kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani ulaya baada ya kutolewa na Real Madrid raundi ya 16 bora.

Manchester United wapo tayari kumuuza mshambuliaji wao Anthony Martial kwa ada ya uhamisho ya pauni miliioni 20 ambayo ni zaidi ya Bilioni 57 kwa pesa ya Tanzania. Martial ana mkataba wa miaka miwili (2) na Manchester United. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa ufaransa hajawa na kiwango bora kwani katika misimu miwili iliyopita amefunga mabao 9 tu kweye michezo 59.

Mabingwa wa Ufaransa klabu ya PSG wapo tayari kumuuza nyota wake Neymar Jr katika dirisha hili la usajili la majira ya joto kama watapata offa nzuri hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Hispania. Kwa sasa PSG wanataka wachezaji vijana zaidi na Neymar mwenye umri wa miaka 30 hawamatazami tena kama mchezaji anayeweza kuwapa mahitaji yao kwa sasa.