Jumanne , 13th Jul , 2021

Bodi ya Ligi Tanzania bara (TPLB) imetangaza kuwa klabu ya Simba ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu bara rasmi watakabidhiwa kombe la ubingwa msimu wa 2020-21, Julai 18 kwenye mchezo wa mwisho wa Ligi, jijini Dar es salaam.

Simba wameshinda ubingwa wa VPL kwa misimu minne mfululizo

Simba walitangazwa rasmi kuwa mabingwa wa VPL msimu wa 2020-21 na ubingwa wa nne mfululizo Jumamosi iliyopita Julai 11 baada ya kuifunga Coastal Unioni ya Tanga kwa mabao 2-0 na kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Mabingwa hao wa Tanznaia wamebakiza michezo miwili ya Ligi dhidi ya Azam FC ndio mchezo unaofata utachezwa Julai 15 na watakabidhiwa kombe  kwenye mchezo wa Mwisho dhidi ya Namungo FC mchezo utakao chezwa uwanja wa Benjamini Mkapa.

Hii hapa taarifa rasmi iliyotolewa na bodi ya Ligi Tanzania bara kuhusu sherehe za kukabidhiwa ubingwa kwa klabu ya Simba SC.

 

 Taarifa ya TPLB