Jumanne , 17th Mei , 2022

Baada ya klabu ya Arsenal kupoteza mchezo wake wa jana usiku dhidi ya Newcastle United kwa magoli mawili kwa sifuri, Wamewapa nafasi nzuri Tottenham na Arsenal kujiweka katika wakati mgumu kuwania kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu ya England msimu huu.

(Wachezaji wa Tottenham wakishangilia goli dhidi ya Arsenal)

Sasa Tottenham hotspurs wamebaki nafasi ya nne na alama zao 68, huku Arseanal wakisalia katika nafasi ya 5 na alama zao 66, hivyo kuwa nyuma kwa tofauti ya alama mbili. Spurs wanahitaji ushindi ama sare katika mchezo wao wa mwisho ili wafuzu kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao, huku Arsenal wakilazimika kushinda mchezo wa mwisho na wakati huo wakiomba spurs wapoteze mchezo wao wa mwisho ili waweze kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao.

Ligi kuu ya England itafikia tamati mwisho wa wiki hii na Arsenal wamebakisha mchezo dhidi ya Everton wakiwa nyumbani katika uwanja wa Emirates, huku wapinzani wao Tottenham wakibakisha mchezo wa ugenini dhidi ya Norwich City ambao tayari wamesha shuka daraja.